Chama cha ACT – Wazalendo
kimetangaza azma yake ya kufanya mkutano mkuu wa kidemokrasia Jumamosi
ijayo licha ya kuwapo kwa amri ya Polisi iliyokataza kufanyika kwa
mikutano yote ya kisiasa nchini.
Jeshi la Polisi lilipiga marufuku
maandamano na mikutano yote ya hadhara tangu Juni 7 hadi pale hali ya
usalama itakapotengemaa.
Jeshi hilo lilisema limefikia hatua hiyo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa vyama vya siasa vikitaka kufanya mikutano na maandamano kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi.
Lakini jana, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT – Wazalendo, Ado Shaibu alisema wamepanga kufanya mkutano huo kwa sababu Katiba inawaruhusu.
Jeshi hilo lilisema limefikia hatua hiyo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa vyama vya siasa vikitaka kufanya mikutano na maandamano kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi.
Lakini jana, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT – Wazalendo, Ado Shaibu alisema wamepanga kufanya mkutano huo kwa sababu Katiba inawaruhusu.
“ACT
kimekusudia kuitisha mkutano mkuu wa kidemokrasia, hii ni haki yetu
kikatiba na hata kwa dunia nzima si ajabu kwa kuwa vyama vya siasa
hufanya hivyo. Kongamano hili litawaleta pamoja wanachama, wadau na
wafadhili wa ACT ambao watajadili hali ya maendeleo ya nchi,” alisema na kuongeza.
“Hatutaji
mahali na ukumbi tutakaoufanyia kwa sasa, wakati ukifika
tutawajulisha.Na hatutaomba kibali kwa kuwa katiba haisemi vyama vya
siasa viombe kibali vinapotaka kufanya mikutano ya ndani.”
Shaibu
alisema kuwa endapo serikali itazuia kufanyika kongamano hilo
watachukua hatua za kisheria kupinga maamuzi hayo kwa madai kuwa katiba
ya nchi na ya vyama vya siasa inarushusu kufanyika.
“Serikali
ilituzia kufanya mikutano na vikao vya ndani, tulikaa kimya awali
tukiamini kuwa tutaishawishi kwa hoja na itajirekebisa lakini haikufanya
hivyo.Tunaamini serikali itarudi nyuma na kuamini haina mamlaka ya
kuzuia mikutano na vikao vya ndani kwa sababu kuizuia inamaana unafuta
shughuli za siasa na sisi tutakuwa wa mwisho kukubali vyama kufutwa ,” alisema.
Alisema
ACT haitokuwa nyuma kuiunga mkono serikali inapofanya vyema na kwamba
endapo chama hicho kitakosoa utendaji kazi wake, serikali isikichukie
kwa kuwa kinatekeleza wajibu wajibu wake.
Kwa
upande mwingine, Shaibu alisema Kamati Kuu ya Uongozi wa Chama cha ACT
imefanya baadhi ya marekebisho ya muundo wa uendeshaji kwa kuteua baadhi
ya makatibu wa kamati za chama hicho.
“Kikao
cha tatu cha kamati kuu kilichoketi Septemba 5,2016 kilifanya teuzi
mbalimbali za makatibu, sambamba na kugawa baadhi ya kamati ikiwemo
iliyokuwa kamati ya Ulinzi, Usalama na Uadilifu ambapo kwa sasa
imegawanyika na kuwa kamati ya Usalama na Ulinzi na mpya ni Kamati ya
Uadilifu, ” alisema.
Aliwataja
makatibu wapya wa kamati walioteuliwa akiwemo aliyewahi kuwa Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Vijana Chama cha Wananchi CUF (JUVICUF) Mohamed Babu
ambaye kwa sasa ni Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Ally Kifu
ameteuliwa kuwa Katibu wa kamati ya Fedha na Miradi ya Kujitegemea.
Katibu mwingine aliyeteuliwa ni Sabrah Mohamed ambaye ameshikilia
Kitengo cha Kushughulikia Maendeleo ya Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment