Ndege
ya kwanza kati ya mbili zilizonunuliwa na Serikali za Shirika la Ndege
la Tanzania (ATCL), inatarajiwa kuingia nchini kesho ikitokea Canada.
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Patrick Itule alisema ndege hiyo aina ya
Bombardier Q400 inatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) saa 7:00 mchana.
Itule
alisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 76, tayari imeanza
safari ya kuja nchini tangu mwishoni mwa wiki iliyopita ikipitia miji ya
Reykjavík, Southampton, Malta, Luxor, Addis Ababa Ethiopia kabla ya
kutua nchini ikiwa na timu ya marubani wanne kutoka Canada.
0 comments:
Post a Comment