SI mbilikimo tu..!! Bali Laura Whitfield (26) mwenye urefu wa futi 4 na nchi 2 pekee,ni Mwenza waNathan Phillips (37) mwenye urefu wa futi 3 na na nchi 11.
Raia hao wa Uingereza waliochumbiana kabla kuzaliwa kwa mtoto wao Nathan Jr,ambae uchunguzi wa kitabibu ulieonesha kuwa mtoto wao ana umbilikimo mara dufu ukilinganisha na wazazi wake kutokana na kuwa na aina mbili za umbilikimo, yaani "anachondaplasia" kama Mama yake na "pseudochondaplasia"kama Baba yake.
Nathan Jr.
Kutokana na hali hiyo, Madaktari walitabiri Mtoto huyo kufariki saa chache baada ya kuzaliwa.
Lakini wahenga walisema; ‘Mungu si Athumani,’ kwani Nathan Jr.kwa sasa ana umri wa miaka miwili na nusu na alikuwa mshika pete wa ndoa ya wazazi wake hao,katika sherehe iliyofanyika kwenye hoteli ya South Causey na kuhudhuiwa na ndugu na marafiki wa karibu 50.
Kwa mujibu wa mtandao wa Telegraph Wenza hawa awali walikutana wakati wakicheza shoo ijulikanayo"Snow White" na walifunga ndoa kanisani ambapo Bibi harusi Laura aliambatana na mwanae na Mumewe kuelekea kanisani akiwa amevalia gauni lenye thamani ya pauni 800 sawa na Sh milioni 2.4.
0 comments:
Post a Comment