Katika
kile kinachoonekana kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha,
Rais John Magufuli amesema kwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili
fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pa kuzipeleka.
Akizungumza
katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa
Mlimani City leo mchana mjini hapa, Magufuli amesisitiza kuwa kauli
hiyo ni mahsusi kwa watu walioficha fedha katika majumba yao na kuwataka
kuachana na tabia hiyo mara moja ili fedha hizo ziingie katika
mzunguko.
Huku
akisisitiza kuwa katika utawala wake fedha za bure hazitakuwepo kwa
sababu zilizokuwepo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serikalini
ambazo kwa sasa zimedhibitiwa, alisema kwa mwendo anaokwenda nao sasa ni
ngumu kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi.
0 comments:
Post a Comment