Ikiwa unahitaji mahusiano ya kudumu na mwanamke mmoja huna budi kujiepusha na wanawake wa aina hii.
Anaenda maisha ya starehe.
Unakutana na mwanamke ambae kila siku ya weekend yuko katika klabu za usiku na huwa na rafiki zake wa kike wakinywa pombe, wakivuta bangi, shisha au sigara na wala huoni muda analipa bili then unaona picha zake akiwa na rafiki zake na ukiangalia kwa makini utamwona akiwa na marafiki tofauti wa kike na kiume katika kila picha kwenye mitandao yake ya kijamii,basi jua huyo siyo mtu mwenye malengo au mipango ya muda mrefu.
Uhusiano wa karibu na wanaume tofauti.
Mwanamke wa aina hii mara nyingi anaweza kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaume tofauti kwa wakati mmoja.Kazi yake kubwa ni kujisifu kwa wenzie kuhusu mahusiano yake na wanaume hao ambao yuko nao na kuchat nao kwenye simu wakati wote. Sio muda wote ataweza kujibu text zako au kupokea simu zako kwa wakati na atakupa visingizio vingi tu, yule rafiki yangu tu, yule nafanya nae kazi, yule tumekuwa wote mtaani.Kuna wakati inaweza kuwa kweli lakini lazima kuna mtu katika hao aliokupa maelezo yake ambaye tayari ameshakuwa nae,yuko nae,au ana mipango ya kuwa nae kimapenzi.
Hujitongozesha/Hujilengesha.
Na kwa tabia hii, hujikuta yuko kwenye mahusiano na mwanamume aliye na familia ama mwenye mchumba anayetaka kumuoa.Pia haokupi kutoka kimapenzi na mume wa rafiki yake au dada yake.
Hizi ni baadhi ya nyimbo zinazopendwa na Wanawake wa aina hii :
Freak like me – Adina Howard
I’m a survivor- Destiny’s Child
Miss Independent – Neyo
Irreplaceable- Beyonce
Single Ladies- Beyonce
Girl on Fire- Alicia Keya
No scrubs- TLC
I’m every woman- Chaka Khan
0 comments:
Post a Comment