Na Anna Nkinda - JKCI
Serikali
ya Kuwait imeahidi kuisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
vifaa vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji wa damu , mashine na
vifaa vya upasuaji ambavyo vitatumika katika chumba cha upasuaji.
Ahadi
hiyo imetolewa leo na Balozi wa nchi hiyo Mhe. Jasem Al Najem
alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia ni jinsi gani nchi
yake inaweza kuisaidia katika upatikanaji wa vifaa tiba.
Mhe.
Balozi Al Najem alisema vifaa vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji
wa damu vitapatikana kabla ya kumalizika kwa mwaka huu ambapo vifaa
pamoja na mashine za upasuaji vitapatikana mwanzoni mwa mwaka ujao wa
2017.
“Serikali
ya nchi yangu inaangalia namna ya kushirikiana zaidi na Taasisi hii
pamoja na Taasisi zingine zilizopo Dar es Salaam, Zanzibar na maeneo
mengine hapa nchini ili watanzania waweze kupata huduma bora”, alisema
Mhe. Balozi Al Najem.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi
alishukuru Serikali ya Kuwait kwa kuahidi kuwapatia vifaa pamoja na
mashine zitakazotumika katika matibabu ya wagonjwa wa moyo.
“Tuna
vyumba vitatu vya upasuaji, vinavyotumika ni viwili kwani kimoja hakina
vifaa, kupatikana kwa vifaa pamoja na mashine kutoka nchini Kuwait
kutatufanya tuwe na vyumba vya upasuaji vitatu ambavyo vitasaidia kutoa
huduma ya upasuaji kwa wagonjwa .
Akiwa
katika Taasisi hiyo Mhe. Balozi Al Najem alitembelea vyumba vya
upasuaji wa moyo, chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum
(ICU) na kutoa zawadi kwa watoto waliolazwa.
Daktari
Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Peter
Kisenge akimuelezea takwimu za upasuaji wa wagonjwa wa Moyo zinazofanywa
na Taasisi hiyo Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem (kushoto).
Wapili kulia ni Dkt. Barjces Almutairi kutoka Mfuko wa Kusaidia wagonjwa
wa nchini Kuwait akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Moyo Tulizo Shemu
Sanga.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed
Janabi akiongea jambo na Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem
wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam
ili kuona namna gani nchi yake inaweza kusaidia vifaa tiba.
Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya gari na ndege ya
kuchezea Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo huku Mama yake
Jumanne akishuhudia.
Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiongea jambo na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed
Janabi wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi hiyo na kuahidi
kuisaidia vifaa vya kutunzia damu na kununua vifaa kwa ajili ya upasuaji
wa moyo katika chumba cha upasuaji. Kulia ni Daktari Bingwa wa Moyo
Peter Kisenge.
Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya mdoli Mtoto
Furaha Mwechi ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo kwa ajili ya kuziba tundu la
moyo na kufungua mshipa wa damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye mapafu.
Mhe. Balozi Najem alitembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam ili
kuona ni jinsi gani nchi yake inaweza kuisaidia vifaa tiba.
Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimkabidhi zawadi ya dawa
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof.
Mohamed Janabi ambazo zitatumika kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi
hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukiza kutoka
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Prof. Ayoub
Magimba na Kulia ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge.
Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Ubalozi wa Kuwait
mara baada ya kumalizika kwa ziara yake aliyoifanya katika Taasisi hiyo.
Kulia kwa Mhe. Balozi ni Mkurugenzi Mtendaji JKCI Prof. Mohamed Janabi.
Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akisaini kitabu cha wageni
alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es
Salaam ili kuona ni jinsi gani nchi yake itakavyoisaidia Taasisi hiyo.
Kulia kwa Balozi ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi.
Picha na Anna Nkinda – JKCI.
0 comments:
Post a Comment