https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Agizo la serikali lakausha hekari 200 za mahindi

    Hekari zaidi ya 200 za mahindi na vitunguu kwenye kijiji cha Kangdet wilayani Karatu mkoani Arusha zimekauka kwa kukosa maji baada ya serikali kuagiza kuondolewa kwa mashine za kuvuta maji zinazodaiwa kuwekwa kwenye vyanzo vya maji pamoja na mto.
    yanavyokusanywa kwenye mrefeji kabla yakuelekezwa kwenda kwenye kisima cha kijiji cha Jobaj, akiwa katika ziara yake hivi karibuni wilayani Karatu
    Wananchi wa kijiji hicho wamelalamikia hatua hiyo ya serikali na kudai kuwa itasababisha kuyumba kwa uchumi pamoja na kukosa chakula katika msimu huu.
    Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mashamba hayo yaliyoathirika pamoja na mkutano mkuu wa kijiji hicho, wananchi hao wamesema kuwa wamekuwa wakitumia vyanzo hivyo kwa muda mrefu katika kilimo cha umwagiliaji.
    Moja kati ya masoko wilayani Karatu
    Mmoja wa wakulima hao Halima Hamisi,amesema hawana tegemeo lingine zaidi ya kilimo hicho cha umwagiliaji na kuwa wengi wao wakiwa wamechukua mikopo kutoka taasisi mbalimbali za fedha pamoja ikiwemo Saccos na Vicoba.
    Amesema kuwa kutokana na agizo hilo la serikali mazao mengi yamekauka huku wananchi hao wakitegemea kilimo hicho cha umwagiliaji kwa ajili ya chakula na biashara ambapo kutokana na eneo hilo kuwa na ukame,wanalazimika kulima kilimo cha umwagiliaji.
    Akizungumzia suala hilo Mkuu wa wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo amesema kuwa siyo kweli kuwa mashine ziliondolewa sehemu zote na wananchi hao ndiyo waliomba mashine hizo ziondolewe kwenye chanzo cha maji na kudai kushangazwa na malalamiko hayo,na kuwa mashine 26 zilizokuwa kwenye vyanzo viwili chemchemi inapoanzia na kwenye mto ambako maji hayo hutiririka ndiyo zilitolewa.
    Amesema wananchi walilalamika hali siyo nzuri na hawapati maji ya kutosha,sheria imechukuliwa wameanza pia kulalamika,mashine zilizotolewa si kweli kwamba mashine zimetolewa katika maeneo yote huo ni uongo, ameomba wananchi wawe wakweli, mashine zilitolewa kwenye chanzo ambacho wanaita jicho na kwenye mto.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Agizo la serikali lakausha hekari 200 za mahindi Rating: 5 Reviewed By: news
    Scroll to Top