Crystal Palace 1-2 Manchester United
Goli la dakika ya 88 kutoka kwa Zlatan Ibrahimovic liliipa Manchester United alama zote tatu dhidi ya Crystal Palace na kufikisha alama 27 ndani ya ligi ya primia.
MAMBO YALIKUWAJE:
1. Katika magoli 11 ya Manchester United yaliyopita (pamoja na magoli ya leo) Ibrahimovic amefunga magoli sita kati ya hayo, pamoja na kuwa na umri wa miaka 35 bado Ibra ameonyesha dhahiri kwamba BADO WAMO. Na hata ukiangalia namna alivyofunga goli la ushindi unabaki kujiuliza hivi Ibracadabra ana miaka 35 ama 25. Bonge ya mshambuliaji ile sanamu kule Sweden inamstahili.
2. Baada ya goli la Ibra kama ulitazama kwa makini benchi la United likiongozwa na Mourinho walishangilia kwa namna ya pekee na baada ya pia ya filimbi ya mwisho Mourinho aliingia uwanjani huku akiwa amekunja ngumu na kuzidi kushangilia, msimu huu mara chache sana hayo yalitokea, USHINDI wa leo ukiwa ni wa pili mfululizo ni kitu kikubwa sana kwa KESHO ya Mourinho na United yake. Ushindi wa UGENINI huipa timu "confidence" kuelekea mbele.
3. Wilfried Zaha naona sasa AMEKUA, utoto ameweka kando na kaamua kucheza mpira, akizidisha pafomansi yake hasa kwenye eneo la mwisho pauni nyingi zinaweza kuhusika kumng'oa pale Selhurst Park. Nyuma ya PAZIA Zaha anapiganiwa na nchi mbili za Uingereza na Ivory Coast, kila mmoja anamtaka na winga huyu anaweza kuchezea kati ya nchi hizi mbili.
0 comments:
Post a Comment