Mamlaka
ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA, leo December 14 imefanya Ukaguzi
wa mwisho, Kujiridhisha na Kuruhusu Kituo cha Utangazaji cha Radio5
Arusha kurudisha Matangazo yake hewani ifikapo December 16 mwaka huu
2016.
Akiongea
na Viongozi na baadhi ya Wafanyakazi wa Radio5 baada ya kukamilisha
ukaguzi wao, Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Fredrick Ntobi amesema wao
kama Mamlaka Waliamua kuja kufanya ukaguzi wao kwa ajili ya
kujiridhisha kurudisha Matangazo ya Kituo hicho hewani December 16
ambapo ndiyo tarehe rasmi ya kuisha kwa Adhabu waliyokuwa wamewapa Kituo
hicho.
Mamlaka
hiyo ilifanya ukaguzi wa Studio ya Kurusha Matangazo (On air Studio),
Studio ya kuzalisha Vipindi (Production Studio), Chumba cha Habari (News
room), Control Room, ofisi zote za Kituo pamoja na Mnara wa Kurushia
Matangazo ambapo kote wamekuta kila kitu kiko sawa kwa kazi kama Mamlaka
inavyotaka.
Hata
hivyo Bw. Fredrick Ntobi akiwa ameongozana na Viongozi wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania TCRA kanda ya Kaskazini, amewakumbusha Watangazaji
na Waandishi kufuata Maadili ya uandishi wa habari ili kulinda Vituo
vyao na Kulinda taaluma zao kwa ajili ya kuendelea kuhabarisha na
kuelimisha Jamii nzima ya Watanzania.
“Mimi
niwasisitize tu kuendelea kufuata maadili ya taaluma yenu ya uandishi wa
habari, kufuata sheria na kanuni za uandishi wa habari ambao mmesomea,
tumieni lugha Sanifu ambayo inakubalika kwa jamii na tasnia yenu na
niwatakie maandalizi mema ya kurudi hewani pamoja na Sikukuu
zinazokuja”. Alimaliza kwa Msisitizo Bw. Fredrick Ntobi.
Hata
hivyo kwa upande wa Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayomiliki
kituo cha Radio5, Bw. Robert Francis, Amewataka Wasikilizaji wa Radio5
kukaa mkao wa Kuhabarika, Kupata Burudani na kuelimika zaidi kupitia
Radio5 kwani Wamejipanga vyakutosha kurudi hewani kwa Kishindo.
“Mimi
niwaombe tu wasikilizaji wetu ambao najua wametumiss sana, wakae tayari
Kuhabarika, kuelimika na kuburudika zaidi sababu mimi na Wafanyakazi
wangu tumejipanga vya kutosha haswa ukizingatia kwamba mwaka mpya ndo
huu unakuja. Kingine niwape pole tu wasikilizaji wetu wote kwa
kutotusikia hewani kwa kipindi cha miezi mitatu, pamoja na Wadau ambao
tumekuwa tukishirikiana kwa pamoja katika mambo mbali mbali niwaambie tu
tunarudi rasmi Ijumaa ya tarehe 16 December 2016”. Alisema Mkurugenzi
wa Radio5 Robert Francis.
Kituo cha Radio5 Kilisimamishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kurusha matangazo yake tarehe 16 September 2016.
Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Fredrick Ntobi wakizungumza jambo na
Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio5, Bw.
Robert Francis,ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA, leo
December 14 imefanya Ukaguzi wa mwisho, Kujiridhisha na Kuruhusu Kituo
cha Utangazaji cha Radio5 Arusha kurudisha Matangazo yake hewani ifikapo
December 16 mwaka huu 2016.
0 comments:
Post a Comment