Kijana kutoka nchini Afghanistan aliyepata umaarufu sana mtandaoni alipopigwa picha akiwa amevalia karatasi kama jezi ya Lionel Messi mechi amefanikiwa kukutana na shujaa huyo wake.
Picha ya Murtaza Ahmadi, mwenye miaka sita, akiwa amevalia karatasi hiyo iliyoandika nambari ya jezi ya Messi pamoja na jina lake ilivuma sana mwezi Januari mtandaoni.
Mwishowe, alipokea jezi halisi kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona, ambayo pia ilikuwa imetiwa saini na mchezjai huyo.
Sasa, wawili hao wamekutana ana kwa ana mjini Doha, kwa mujibu wa kamati andalizi ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.
Barcelona wamo nchini Qatar kucheza mechi ya kirafiki na Al Ahli Jumanne na Ahmadi anatarajiwa kutembea kuingia uwanjani akiandamana na Messi.
“Ni picha ambayo ulimwengu ulitaka kuona,” aliandika mkuu wa kamati hiyo Jumanne.
“Mvulana wa miaka sita akikutana na shujaa wake, #Messi, ndoto yake ikitimia.”
Ahmadi, ambaye anatoka wilaya ya Jaghori, katika mkoa wa Ghazni mashariki mwa Afghanistan, alilazimika kukimbilia nchi jirani ya Pakistan mwezi Mei
Murtaza alitambuliwa kama mvulana ambaye picha yake ilikuwa ikisambazwa mtandaoni baada ya mjomba wake Azim Ahmadi, raia wa Afghanistan anayeishi Australia, kuwaunganisha waandishi wa BBC Trending na nduguye, Arif – babake shabiki huyo mkubwa wa Messi.
0 comments:
Post a Comment