Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemnyima dhamana Mbunge wa Arusha
Mjini (CHADEMA) Godbless Lema. Mahakama hiyo imeeleza kuwa mawakili
wamtuhumiwa huyo walipaswa kuonesha kusudio la kukata rufaa ndani ya
siku10 kabla ya kukata rufaa.
Hii ni mara ya tano mbunge huyo anakosa dhamana mahakamani tangu
alipokamatwa Novemba 3 mwaka huu akiwa mjini Dodoma na kusafirishwa hadi
Arusha katika kesi ya uchochezi inayomkabili.
Katika kesi ya msingi lema anatuhumiwa kutoa maneno ya kichochezi
dhidi ya Rais Magufuli kwa madai kuwa Mungu ndiye aliyemwambia maneno
hayo wakati akiwa anaomba.
0 comments:
Post a Comment