Mara nyingi watu wamekuwa waoga kwenye matumizi ya zana za online, haswa pale panapokuja kuwa kuna zana zaidi ya moja inayofanya kitu kinachofanana. Hii hutokana na wengi kuogopa kukosea au kupata hasara.Pia, wapo wanaoogopa kujaribu. Instagram ni moja kati ya Website inayotumika sana kwa ajili ya kutangaza biashara.
Wafanya biashara wengi wamekuwa wakitumia Instagram, mfano, kwa hapa nyumbani tumeona watangazaji au watu maarufu wamekuwa wakiweka matangazo ya biashara ya kulipwa, mfano wa hawa ni Millard Ayo na matangazo yake ya Tigo. Pia, Instagram sasa wamekuja na mtindo mpya wa matangazo ambapo tangazo moja linaweza kuonekana kwenye chaneli zao zaidi ya moja, mfano sasa unaweza kuweka tangazo kwenye Facebook na pia likaonekana kwenye Instagram.
Je ushawahi kujiuliza, kwanini kuna bashara zinafanikiwa sana kwa kujitanganza kwenye Instagram wakati nyingine zimekuwa zikifeli? leo tutaliangalia hili. Kuna makosa mengi ambayo watu hufanya kwenye kuitumia Instagram kibiashara, kumbuka kuna utofauti pindi unapoitumia Instagram kwa matumizi yako binafsi na pale unapoitumia kwa biashara. Kwa kuyatambua makosa haya, na kuyarekebisha, basi utaweza kufanikiwa kwenye biashara yako.
1. Utambulishi wa biashara usiokamilia (Bio). Hii itakufanya watu washindwe kujua wewe ni nani na na unafanya nini. Wateja wanahitaji kukufahamu kabla kuwa wateja.
2. Kutofuatilia wanaokufuata. Ingawa si lazima uwafuate wote, lakini lazima kuwe na uhusiano mzuri kari ya wewe na wateja wako na kuwafuata (follow) kadri uwezavyo. Pia, hapa unatakiwa kuchunga, nani wa kumfuata na nasi si wa kumfuata.
3. Kutotuma kwa mpangilio. lazima ujiwekee utaratibu wa kutuma picha na matukio kwenye instagram. Siyo unatuma kila kitu. pia hakikisha unatumia pich zenye ubora. Instagram ni picha na picha ni Instagram, hivyo suala la ubora wa picha ni lazima uliwekee umuhimu.
4. Maumizi ya hashtag. Hakikisha unatumia hashtag kimpangilio. Mfano, Dudumizi tuna hashtags zetu kama #thinkinnovate #du16, hivyo hashtag hizi n lazima ziwe na maana na pia kuwe na muendelezo, siyo kila siku hastag mpya. Pia unaweza kutumia hashtag zenye huduma unayotoa au brand yako, mfano #dudumizi. Kabla ya kutumia hashtag, ni vyema ukafanya utafiti wa matumizi ili isije kuingiliana na nyingine zenye matumizi yasiyofaa.
5. Kutuma sana au kutuma kidogo. Hpa unatakuwa kutafuta uwiano wa utumaji wa makala, usitume sana wala kidogo. Kwa kutuma sana utasababisha watu wakuone spam, na kutuma kidogo utafanya watu wakusahau.
6. Kila siku ni kazi. Ingawa unatumia Instagram kwa ajili ya biashara, lakini watu hawataki kila siku waone picha za vikapu au batiki. Kuwa mbunifu wa aina ya picha unazoweka. Kwanini leo usituwekee picha ya shama ya malighafi za kikapu (ukili), au ukatuwekea picha za namna unavyoandaa batiki. Mchanganyiko huu utaifanya Instagram yako iishi maisha ya uhalisia na si matangazo tuu.
Hizi ni tips kadhaa unazoweza kuzitumia kuboresha matumizi ya Instagram. Ni vyema ukafanya utafiti kabla haujaanza kutumia Instagram kibiashara. Pia, hakikisha unakuwa na mpango mzuri utakaokuwezesha kupata matokeo bora.
0 comments:
Post a Comment