Manchester United yaendeleza wimbi la ushindi kwa kuichapa West Brom kwa magoli mawili kwa bila, magoli yote mawili yakifungwa na Zlatan Ibrahimovic. Huu ukiwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Manchester United kushinda.
1. JINA: Zlatan Ibrahimovic
UMRI: Miaka 35 ama "25".
MAGOLI: 10 Ndani ya michezo tisa na 16 mpaka sasa ndani ya msimu huu.
Kwasasa Ibracadabra ndiyo jina ambalo litakuwa linatamkwa sana kwenye viunga, vijiwe na pub za jijini Manchester huyu ndiye ambaye anaifanya Manchester ionekane kurejea kwenye enzi za ushindi mfululizo. UHUSIANO wa Ibra na Mou toka kitambo ni dhahiri unaleta matunda ndani ya himaya ya mashetani wekundu.

2. Jose Mourinho kama huko nyuma alikuwa hajui nani ampange wapi na kwanini basi kwasasa ni dhahiri anaijua timu yake bora ni ipi na kwasasa United wanaonekana wazi kuwa inafinyangwa kwa udongo wa "kispecial one" hasa kwa namna ambavyo wanazuia (defending) kufungwa. KESHO ya Mourinho sio mbaya kuifikiria. NA PIA WAYNE ROONEY KWASASA ANAELEWEKA.
3. Tony Pulis bado anapendwa pale Hawthorns, pamoja na kupoteza mchezo wa leo bado aliendelea kuimbwa na mashabiki wa Baggies, uzuri wa Pulis ni kwamba atafungwa na timu vigogo lakini anapokutana na "size" yake huwa hana simile, anachukua alama zake tatu na kujifariji. Alama 23 na nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi sio mbaya kwa timu ya aina yake.
0 comments:
Post a Comment