Waziri wa
fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango akizungumza na waandishi wa habari
juu ya ukuaji wa uchumi wa nchi kutokana kuongezeak kwa uzalishaji wa
chakula na mazao mbalimbaliu ya kilimo, biashara, viwanda na migodi.
Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii.
Takwimu
za ukuaji wa uchumi nchini unaonyesha unaendelea kukua kwa kiasi kubwa
zaidi kulinganisha na mataifa mengine na kuwa miongoni mwa Nchi za
bara la Afrika , Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unakuwa
ikifuatiwa na Congo DRC na Rwanda,Kenya, Uganda, Burundi, Afrika ya
Kusini, Zambia na Malawi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Waziri wa fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango
amesema kuwa kukua kwa uchumi kunapimwa kwa kuangalia shughuli
mbalimbali za kiuchumi zikiwemo ni pamoja na uzalishaji wa chakula na
mazao mbalimbali ya kilimo, mifugo na uvuvi, uzalishaji wa bidhaa za
viwandani na migodini, ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma
mbalimbali za kwa jamii ikiwemo afya, elimu na maji.
"Kasi ya
kuongezeka au kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa na huduma katika nchi ni
mojawapo ya vitu vinavyotazamwa katika kutathmini afya ya uchumi wa
Taifa kwa ujumla ambapo kiashiria kimojawapo kinachotumika kupima ukuaji
wa uchumi ni ukuaji wa pato la Taifa."
Aidha Dkt
Mpango ameongeza kuwa kiashiria kingine ni mfumuko wa bei bao unapima
mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya ambapo
ulipungua kutoka asilimia 6.5 januari 2016 hadi asilimia5.5 juni na
kupungua zaidi hadi kufikia asilimia 4.5 na kupanda hadi asilimia 4.8
mwezi novemba 2016.
Amesema
katika mwezi huo wa Novemba takribani nchi zote zilikuwa na ongezeko la
mfumuko wa bei kutokana na kuyumba kwa ugavi wa chakula katika nchi ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupanda kwa bei kwa bei za mafuta katika
soko la Dunia.
Dkt
Mpango amesema kwa tathimi ya upande wa mabenki unaonyesha kuwa benki
yanaendelea kuimarika huku yakiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha kwa
kuangalia uwiano kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu
na amana zinazoweza kuhitajika katika muda mfupi ambao ulikuwa kwa
asilimia 37.46 ukilinganishwa na uwiano wa chini unaohitajika kisheria
wa asilimia 20.
" amana
za wateja katika benki zilipungua kidogo kutoka Trilioni 20.73 mwezi
Desemba 2015 kufikia shilingi Triliani 20.57 mwezi septemba kutokana na
uamuzi wa Serikali kuhamisha sehemu ya fedha za taasisi na mashirika ya
Umma kutoka benki ya biashara kwenda benki kuu ya Tanzania."
Hata
hivyo Mpango amesema kwa kuzingatia mwenendo wa ukuaji wa uchumi kwa
kipindi cha Januari hadi septemba 2016 matarajio ni kwamba kasi ya
ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2016 na 2017 unatarajiwa kufikia hadi
asilimia 7.2 kama ilivyokaririwa awali.
Waandishi na watumishi mbalimbali wa sekta ya fedha nchini wakimsikiliza
Waziri wa fedha na Mipango Dkt Phillip Mpango ahyupo pichani.
Picha na Chalila Kibuda.
0 comments:
Post a Comment