MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 8.5%.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi, (pichani),
ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini,
(TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei
kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017.
Akitangaza
bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA
amesema, baada ya kufanya uchambuzi wa kina, Mamlaka yake imefikia
uamuzi wa kuongeza asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017
kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake.
Shirika
la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka
Zanzibar limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme.Hata hivyo
ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao
hayazidi uniti 75 kwa mwezi.Kundi la TIB linalohusisha viwanda vidogo,
mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi
5,520.
Shirika
la Umeme Tanzania, (TANESCO), linaendelea kufanya maboresho ya
miundombinu ya umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja
ili kuboresha huduma za umeme nchini.
0 comments:
Post a Comment