KESI ya
uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake, imeahirishwa hadi Januari 20
mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.
Wakili
Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi alidai jana katika Hakimu
Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri kuwa kesi imekuja kwa
ajili ya kutajwa na kwamba hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Cyprian
Mkeha, hayupo.
Kishenyi
alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo aliomba tarehe
nyingine kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Mashauri alikubaliana na ombi hilo
na kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 20 mwaka huu. Katika shauri
lililopita, Hakimu Mfawidhi, Mkeha aliutaka upande wa mashitaka kueleza
upelelezi wa kesi hiyo umefikia hatua gani.
Wakili
Esterzia Martin alidai kuwa jalada la kesi hiyo lipo Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa ajili ya kuendelea kuchunguza
nyaraka.
Hivyo,
aliomba apangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kueleza upelelezi umefikia
wapi. Mbali na Kitilya, wengine ni mshindi wa Mashindano ya Urembo
(Miss Tanzania) mwaka 1996, Shose Sinare na Mwanasheria wa Benki ya
Stanbic, Sioi Solomon. Kwa pamoja, washtakiwa hao wanakabiliwa na
mashtaka manane, likiwemo kutakatisha fedha, dola za Marekani milioni
sita.
Wanadaiwa
kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi 2013 na
Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa Dola za Marekani milioni
550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.
0 comments:
Post a Comment