Agizo
la Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dr. John Pombe Magufuli la kulitaka
jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kung’oa matairi vyombo
vyote vya moto vitakavyopita katika barabara za mabasi yaendayo haraka
limeanza kutekelezwa kwa vitendo ambapo pikipiki kumi na sita
zimeng’olewa matairi na wahusika wakitarajiwa kufikishwa mahakamani
tarehe 2 Febuari mwaka huu.
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alisema kuwa pikipiki
hizo 16 zilizotolewa matairi ni sehemu tu ya nyingi zilizokamatwa huku
akisema kuwa mkakati huo ni endelevu ambapo wote watakamatwa na
kufikishwa mahakamani.
Rais
Dkt Magufuli alitoa maagizo kwa askari kukamata magari na pikipiki
zinazotumia barabara za mabasi yaendayo haraka na kisha kuzitoa matairi
na madereva hao wafikishwe mahakamani. Rais Magufuli alisema madereva
hao wakiuliza matairi yao yalipo, wajibiwe kuwa askari hawajaajiriwa
kulinda matairi.
0 comments:
Post a Comment