Mwimbaji
Mtanzania Diamond Platnumz alikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa
michezo na sanaa Nape Nnauye baada ya kualikwa kutumbuiza kwenye
ufunguzi wa michuano ya soka ya Afrika 2017 kwenye taifa la Gabon.
Baada
ya hapo Ridhiwani aliandika kuhusu timu ya taifa ya soka ambapo wengine
waliitafsiri post yake kama amechukia Diamond kupewa bendera lakini leo
kupitia The Beauty TV amehojiwa na kutoa ufafanuzi.
"Kwanza
watu wanatakiwa kuelewa kwamba ile post haikuwa kwasababu ya Diamond na
hata ukisoma kwenye maandishi yangu hakuna sehemu Diamond ametajwa
isipokua msg iliyo pale inaweza kuwa inamgusa Diamond.
"Kilichonifanya
niandike ile msg ni ule wivu wa kuona kwamba mashindano yanayokwenda
kufanyika ni ya mpira wa miguu, sisi tunayo timu ya taifa ya mpira wa
miguu lakini kilichotushangaza badala ya kutoa bendera kwa timu ya mpira
wa miguu tunawapa Waburudishaji kina Diamond
"Matarajio
yetu sisi watu wa mpira ni kuona Nahodha wa timu ya taifa akipokea
Bendera, aliyepaswa kupokea bendera ni captain wa timu ya taifa……. hii
pia lakini ni kuwapa changamoto TFF, je wao wanashangilia kuona Diamond
amepewa bendera?
"Mtazamo
wangu mkubwa ulijikita huko na sio mtazamo wa kwamba Diamond sijui
nani………. NO NO… Diamond yeye nampongeza sana kwa hatua aliyofika,
anafanya kazi nzuri na ndio maana watu wamemuona wamempa nafasi ya
kwenda kutumbuiza lakini kikubwa ni nini ajenda kubwa Gabon? ajenda ni
mpira wa miguu.
"Diamond
sio mcheza mpira wa miguu, hata kama anashabiki atakua ni mshabiki tu….
sisi kama Mashabiki wa soka tunaona wenzetu wanajiandaa kuhakikisha
timu zao zinafuzu kwenda kucheza katika hatua ile, sisi kwetu tunaandaa
Wanamuziki kwenda kuburudisha, ni jambo la kusikitisha sana"
0 comments:
Post a Comment