Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata (kulia) akifurahi jambo na
Meneja Mauzo wa Tigo Moses Busee mara baada ya kuonyesha laini ya 4G intaneti |
zitakazotumika kwenye mashindano ya Killi Marathon yaliyodhaminiwa na Kampuni hiyo.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo imeendelea kuboresha huduma ya mtandao wake wa wenye kasi kubwa wa 4G kanda wa kaskazini mwa Tanzania hatua inayolenga kuwarahisishia wateja wake wa maeneo hayo na wageni
kutoka mataifa mbali mbali wakiwemo watakaoshiriki katika mashindano ya kimataifa ya Kilimanjaro Marathoni yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi February katika mji wa Moshi.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni hiyo Bw George Lugata amesema katika kuhakikisha kuwa lengo hilo linafikiwa kampuni imeanza kuongeza minara ya mawasiliano ya mtandao wa 4G maradufu na maeneo mengi kwa sasa wateja wao wameendelea kupata huduma hiyo hiyo
"Kama mnavyojua kampuni ya Tigo ndio wadhamini wakuu wa mbio hizo kwa upande wa kilomita 21 na kama mnavyojua mashindano haya yanawaleta pamoja watu kutoka mataifa mbali mbali ambao kwao wanatumia mitandao yenye kasi kubwa sasa tunataka wasipate shida na wajisikie wako nyumbani kwao na waweze kutuma picha na video kwa urahisi'Alisema Bw, Geoge Lugatamkurugenzi wa mawasiliano Tigo kanda ya kaskazini
Baadhiya wateja wanaotumia mtandao wa huo wa 4G ambao una kasi kubwa wamesema umewarahisishia kazi zao na kuwaokolea muda na gharama za kusubiri wakati wanapohitaji kupakua na kutuma picha na video na wameipongeza Tigo kwa kuboresha huduma na kuwa karibu na wateja wake
Kimsingi ukitumia Mtandao wenye kasikubwa unaokoa gharama na muda unaotumia kusubiri ukiwa na mitandao mingine , mfano mimi ninapenda sana kupakua na kupakia picha na video na nilivyoanza kutumia 4G kwa kweli nafurahia sana" alisema Bw, Mussa Msemo -Mtumiaji wa Mtandao wa Tigo 4G
|
0 comments:
Post a Comment