WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli
hajawahi kutangaza ama kutoa kauli ya kufutwa kwa vyama vya siasa
nchini.
Ametoa
kauli hiyo leo (Februari, 2, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu
swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman
Mbowe katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.
Katika
swali lake Mheshimiwa Mbowe alisema Rais Dkt. Magufuli alinukuliwa
akisema atahakikisha anafuta vyama vyama vya upinzani na ifikapo mwaka
2020 hakuna upinzani nchini.
Pia
Mheshimiwa Mbowe alitaka kujua nini kauli ya Serikali kuhusu kunyimwa
dhamana kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema ambaye
anashikiliwa kwa muda miezi mitatu.
Mbali
na Mheshimiwa Lema, pia kiongozi huyo alitaka kujua kuhusiana na
kufungwa kwa Mbunge wa Kilombelo, Mheshimiwa Peter Lijualikali pamoja na
madiwani sita wa chama hicho ambao wamefungwa na viongozi wengine 215
wanakabiliwa na kesi mbalimbali.
“Kwanza
nataka nikanushe kwamba Mheshimiwa Rais hajawahi kutangaza kuvifuta
vyama vya upinzani. Pia Watanzania wote wanajua nchi hii inaongozwa kwa
sheria, kanuni na taratibu i,” amesema Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa “tunajua katika kuendesha nchi tunaendesha kwa
mihimili mitatu ipo Serikali, Mahakama na Bunge na hakuna mhimili
unaoweza kuuingilia mhimili mwingine,”.
“Pia
Watanzania wote wanajua kwamba jambo lolote ambalo lipo Mahakamani
haliwezi kuzungumzwa mahali pengine popote, hivyo siwezi kutumia nafasi
hii kuzungumzia mambo yote yanayoendelea chini ya sheria na yaliyo
mahakamani,” amesema.
Wakati
huo huo; Waziri Mkuu amewahakikishia Watanzania kwamba suala la
upungufu wa sukari halitatokea nchini kwa sababu viwanda vya ndani
vinaendelea kuzalisha na hadi mwishoni mwa Januari vilifikia asilimia 86
ya uzalishaji.
“Hadi
kufikia mwishoni mwa msimu wa uzalishaji ambao ni mwezi Machi, tunaweza
kuwa tumefikia malengo na kama itajitokeza upungufu Serikali itatafuta
namna nzuri ya kupata sukari kwa kushirikiana na wenye viwanda nchini,”
amesema.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mvomero,
Mheshimiwa Suleiman Sadiq aliyetaka kujua hali ya sukari ilivyo nchini
kwa sasa na hatua gani zinazochukuliwa na Serikali ili kunusuru hali ya
uhaba wa sukari isijitokeze.
0 comments:
Post a Comment