CHELSEA leo wanaikaribisha Manchester City katika uwanja wa Stamford Bridge na timu hizi mbili zimekuwa na kiwango kizuri msimu huu.
Mechi hii inayoanza saa 2:30 usiku inatarajia kuwa na msisimko mkubwa kutokana na ubora wa wachezaji wa timu zote.
The Blues chini ya Jose Mourinho itamkosa Cesc Fabregas
anayesumbuliwa na majeruhi pamoja na Diego Costa aliyefungiwa mechi
tatu.
Man City chini ya Manuel Pellegrini wanamkosa Yaya Toure
ambaye anaitumikia Ivory Coast katika michuano ya kombe la mataifa ya
Africa inayoendelea nchini Guinea ya Ikweta.