Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa (kulia) akiondoka na mpira baada ya kumkanyaga Emre Can
PAUL Scholes anaamini kuwa Diego Costa anatakiwa kuigwa kwa uvumilivu wake awapo uwanjani na si kukosolewa kwa kosa alilofanya.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa England amefungiwa mechi tatu kwa kitendo cha
kumkanyaga mchezaji wa Liverpool, Emre Can wakati wa mechi yao ya pili
ya nusu fainali ya kombe la Ligi iliyopigwa jumanne iliyopita uwanja wa
Stamford Bridge.
Baadaye
Costa alijihusisha katika kosa lingine la kumchezea vibaya beki wa
Liverpool Martin Skrtel, lakini FA imesema haitamchukulia hatua yoyote
kutokana na tukio hilo.
Costa akikanyaga mguu wa kulia wa Can
Licha ya
hasira za Costa, gwiji wa Manchester United, Scholes amedai mshambuliaji
huyo wa The Blues anatakiwa kuheshimiwa kufuatia kuchukizwa na Skrtel