na klabu hiyo ya nchini Italia.
Eto’o ambae mwanzoni mwa msimu huu alisajiliwa kama mchezaji huru na klabu ya Everton ya nchini England amefanyiwa vipimo hivyo mjini Roma katika kituo cha afya, Villa Stuart clinic na kuonekana anastahili kuwa sehemu ya kikosi cha Sampdoria.
Akielezea furaha yake baada ya kukamilisha mpango wa usajili huko Stadio Luigi Ferraris mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33, alisema ni hatua nzuri kwake kuendelea kuthaminiwa katika medani ya soka.
Alisema hatua ya kucheza soka nchini italia kwa mara ya pili ameichukulia kama ukurasa mpya wa maisha yake ya mchezo huo ambao kila siku umekua na changamoto mpya uwanjani.
Samuel Eto’o aliwahi kuitumikia klabu ya Inter Milan ya nchini Italia kuanzia mwaka 2009–2011 na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa nchini Italia kisha ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya chini ya utawala wa meneja kutoka nchini Ureno, Jose Mourinho.
“Nimepima afya yangu kwa mafanikio makubwa, sina budi kumshukuru dokta Parfait Ondo, ambaye amethibitisha nipo safi kuendelea kucheza soka hapa Italia, Eto’o aliandika kwenye mndao wa Twitter.
Eto’o ameondoka Goodson Park kama mchezaji huru baada ya kuruhusiwa na viongozi wa klabu ya Everton kwa lengo la kukinusuru kipaji chake, baada ya kuonekana hayupo kwenye mipango ya meneja wa klabu hiyo Roberto Martinez