https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    FABREGAS AFIKISHA ASSIST 15 MISIMU MIWILI

    Fabregas_3179732
    Kiungo wa Chelsea ya Uingereza, Mhispaniola Cesc Fabregas ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutengeneza mabao 15 katika misimu miwili huku akiikaribia rekodi ya kutengeneza mabao 20 yake mkongwe Thierry Henry

     Fabregas alitengeneza nafasi ya 15 jumamosi katika pambano dhidi ya Swansea City ambapo walishinda 5-0 kunako dimba Liberty Stadium huku akikumbukwa kwa kutengeneza nafasi 17 alipokuwa na Arsenal msimu wa  2007-08 katika msimu mabo walimaliza nafasi ya tatu nyuma ya klabu yake ya sasa Chelsea na mabingwa wa msimu huo Manchester United

    Kiujumla kitakwimu Fabregasi ametengeneza goli la 15 akiwa na Cheelsea toka alipohama Barcelona majira ya Kiangazi, amepangwa mara 21 sawa na dakika 1,851 minutes, amefunga goli 2, akijaribu lango mara 18, ametengeneza nafasi 67; amepiga jumla ya pasi 1,807 (ambapo usahihi ni sawa na 87%). Sasa amebakiza nafasi tano kumfikia Henry aliyemudu kufanya hivyo misimu 12 iliyopita.
    .
    na pengine nyota huyo angeweza kufikisha 16 kama siyo Diego Costa kuukosa mpira hatua chache toka lilipo lango la Swansea

    Orodha kamili ya kutengeneza mabao ‘Assist’ kwa msimu mmoja ligi kuu ya Uingereza ni kama ifuatavyo

    Idadi -Mchezaji (Msimu)
    20 – Thierry Henry (2002-03)
    18 – Frank Lampard (2004-05)
    17 – Cesc Fabregas (2007-08)
    16 – Eric Cantona (1992-93)
    15 – David Silva (2011-12)
    15 – Steve McManaman (1995-96)
    15 – Matt Le Tissier (1994-95)
    15 – Robert Pires (2001-02)
    15 – David Beckham (1999-00)
    15 – Cesc Fabregas (2014-15)
    15 – Nobby Solano (1999-00)
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: FABREGAS AFIKISHA ASSIST 15 MISIMU MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top