Brendan Rodgers (kulia) akimkumbatia Jose Mourinho kabla ya mechi ya ligi kuu England msimu uliopita
Brendan
Rodgers amekiri kuwepo kwa upinzani mkubwa baina ya Liverpool na
Chelsea na hii inamaanisha yeye na Jose Mourinho hawawezi kuwa marafiki
tena.
Timu
hizi zinakutana Anfield leo usiku katika mechi ya kwanza ya nusu
fainali ya kombe la Capital One kuitafuta nafasi ya kucheza
fainali Wembley.
Hata
hivyo Meneja wa Chelsea, Mourinho amejitahidi kurudisha amani kwa
kuwaambia mashabiki wa klabu hiyo ya London waache kuimba nyimbo za
kumbeza Steven Gerrard.
Mourinho
alimsaidia Rodgers kukuza uwezo wake wa ukocha kufuatia kumpa kazi
katika klabu ya Chelsea mwaka 2004 na alimshauri kuchukua kazi Anfield
wakati alipowindwa na Fenway Sports Group mwaka 2012.

