MKOMBOZI wa Simba katika mechi ya
fainali ya kombe la Mapinduzi iliyopigwa uwanja wa Amaan usiku huu,
Mjini Zanzibar, Ivo Philip Mapundo amejawa na furaha kubwa baada ya
kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa kufuatia kudaka penalti ya Vicent
Barnabas iliyowapa ushindi.
Akizungumza kwa furaha na mtandao
huu baada ya mechi kumalizika Ivo alisema: “Mwalimu aliniamini,
akaniingiza dakika za majeruhi kwa lengo la kudaka penalti. Kitu cha
kwanza nilichowaza ni kutokumuangusha mwalimu. Kwali nimefanya vizuri,
nina furaha sana”.
Kipa huyo alisema katika siku
tatu alizofanya mazoezi, mwalimu alimuona katika mazoezi ya kudaka
penalti na akamwambia kuwa kama itafikia hatua ya matatu angemtumia.
Pia amewataka wanasimba kuwa na umoja katika kipindi hiki kizuri kwani kuwa na migongano kutaishusha timu.
“Kikubwa wanasimba wawe na subiri, timu ni nzuri na tunaamini tutafanya vizuri katika mechi za ligi”. Aliongeza Ivo

