Hii itakuwa rahisi sana mtu wangu,
hivi mara ngapi umeshawahi kwenda sehemu ukakutana na maandishi ambayo
umeshindwa kuyaelewa?Teknolojia imekuwa msaada kwenye mengi mtu wangu,
pata picha unasafiri kwa mara ya kwanza kwenda China, unaingia
mgahawani, unapewa menu
imeandikwa kichina, unaanzia wapi kwanza? Google wanatusogeza hapa, google translate app
itakusaidia kama unayumia smartphone yako unaweka app hiyo halafu
unaanza kuitumia, mfano unakutana na bango lenye maandishi unafungua
app, unaionyesha camera ya simu kwenye maandishi hayo unapiga picha,
kwenye kioo cha simu inakuonyesha maana ya neno hilo!
Mbali na hivyo app hiyo inaweza
kukutafsiria kwa sauti hata kile ambacho mtu anakiongea, yenyewe inakupa
tafsiri kwa lugha unayotaka.
Ni rahisi tu, hauhitaji kuwa na internet
ili uitumie, ni app ambayo inafanya kazi hata kama huna bundle mtu
wangu, inapatikana bure kwa wanaotumia android na iPhone pia.

