Dereva wa mkuu wa wilaya Manyoni, Singida ajiua
Muonekano wa Dereva
huyo baada ya kujipiga risasi
Dereva wa Mkuu wa
Wilaya Manyoni, Singida amejiua kwa kujipiga risasi kichwani leo, chanzo bado
hakijajulikana japo ameacha ujumbe kuwa asilaumiwe mtu.
Mtandao huu ulimpigia
simu Mkuu wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela alisema amesikia tukio
hilo lakini hakuwa na uhakika. "Naomba mnitafute baadaye nitakuwa na
maelezo ya tukio hilo," alisema.