Hii ajali imetokea jana Ngara Mkoani Kagera baada ya gari ndogo kugonga mwendesha baiskeli aliyekuwa na abiria aliyempakiza na kuwasababishia umauti hapo hapo.
Pichani ni gari hilo dogo aina ya Saloon likiwa limeharibika vibaya baada ya kugonga watu wawili na kufa papo hapo eneo la Lemela Wilayani Ngara.
Baiskeli aliyokuwa anaendesha marehemu/abiria
Miili ya marehemu ikiwa imesitiriwa kando ya barabara.
Ajali hizi mpaka lini jamani?
Kwa barabara kuu za mikoani limekuwa jambo la kawaida magari kugonga waendesha baiskeli na pikipiki,sijui tatizo ni nini?
-Sijui barabara nyembamba kiasi kwamba waendesha baiskeli na pikipiki wanashindwa kuchukua tahadhari mapema!!
- Au ni spidi kubwa ya magari kutokana na uchache wa magari barabarani ambapo kunapotokea hali ya hatari madereva wanashindwa ku-control vyombo vyao!!