https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    EXCLUSIVE: CHEKA AHUKUMIWA MIAKA MITATU JELA KWA KUMPIGA KIBANDA

    CHEKA (KUSHOTO) AKIWA NA SALEH ALLY
    Bondia nyota nchini, Francis Cheka ‘SMG’ amehukumiwa miaka mita jela katika Mahakama ya  mkoani Morogoro.

    Taarifa zilizotufikia punde zinaeleza Cheka amepatikana na hatia ya kushambulia baada ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake.

    Pamoja na kifungo cha miaka mitatu, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakamani hiyo, Said Msuya amemhukumu Cheka kulipa faini ya Sh milioni moja baada ya kumaliza kifungo hicho.

    Cheka amepatikana na hatia ya shambulio dhidi ya aliyekuwa meneja wa baa yake, Bahati Kibanda aliyemshambulia Julai 2, mwaka jana katika Ukumbi wa Vijana Social aliokuwa ameukodi kwa ajili ya kuendesha shughuki za baa zilizokuwa zinasimamiwa na KIbanda.

    Kutokana na kukutwa na hatia, Cheka amekuhukumiwa kwenda jela kwa muda huo na imeelezwa tayari ameshapelekwa kwenye gereza mkoani humo.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: EXCLUSIVE: CHEKA AHUKUMIWA MIAKA MITATU JELA KWA KUMPIGA KIBANDA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top