Mkuu
Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mussa
Jallow (wa tano kulia) akikabidhi msaada wa pikipiki kwa Mwenyekiti wa
Chama cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani Mponda katika
hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2,
kompyuta, kofia na mafuta maalumu ya ngozi vikiwa na lengo la
kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana
na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar
es Salaam jana. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha
albino.
Ofisa
Mkaguzi wa Sheria za Ndani za Benki wa NBC, Lilian Kawa (katikati)
akikabidhi msaada wa kofia kwa Katibu wa Chama Cha Albino Tanzania Mkoa
wa Pwani, Aicha Joakim Ngure (wa tatu kushoto) katika hafla ambayo NBC
pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, pikipiki, kompyuta
na mafuta maalumu ya ngozi ili kuwasaidia na matatizo yanayowakabili
kutokana na tatizo unaotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi.
Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya maofisa
wa NBC na kutoka chama cha albino.
Meneja
wa Benki ya NBC Tawi la Kibaha, Asia Chambega (wa pili kulia)
akikabidhi msaada wa mafuta maalumu ya ngozi kwa mmoja wa wawakilishi
kutoka Chama Cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Haika Ngowo, katika
hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2,
pikipiki, kompyuta na kofia vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo
yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba
kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wengine
ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
Meneja
Udhibiti wa Sheria wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mwanakombo
Joshua (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa kampyuta kwa Mwenyekiti wa
Chama cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani Mponda katika
hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2,
pikipiki , kofia na mafuta maalumu ya ngozi vikiwa na lengo la
kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana
na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar
es Salaam. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha
albino.
Ofisa
Uchunguzi wa Idara ya Udhibiti wa Sheria wa Benki ya NBC, Mathias
Raymond (wa pili kulia) akikabidhi msaada kompyuta kwa mmoja wa
wawakilishi kutoka Chama Cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Haika Ngowo,
katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni
3.2, pikipiki, kofia na mafuta ya ngozi vikiwa na lengo la kuwasaidia
na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi
vinasaba kutoka kwa wazazi. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na
kutoka chama cha albino.
Mkuu
wa Kitengo cha Udhibiti wa Sheria wa NBC, Joyce Mbago (wa tatu kulia)
akikabidhi mfano wa hundi ya sh milioni 3.2 kwa Mwenyekiti wa Chama cha
Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani Mponda katika hafla ambayo
NBC pia ilikikabidhi msaada wa pikipiki , kofia, kompyuta na mafuta
maalumu ya ngozi vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo
yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba
kutoka kwa wazazi.
Baadhi
ya maofisa wa Benki ya NBC, wakiwa na wawakilishi wa Chama cha Albino
Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla hiyo.