Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF Tanzania, Abubakar Rajab, akitoa mada
katika warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii
iliyoandaliwa na Taasisi ya Hifadhi ya Jamii ya Africa Mashariki na Kati
(ECASSA) inayoendelea nchini Mauritius.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF Tanzania, Abubakar Rajab, akimkabidhi
zawadi Mh. Fazila Jeewa waziri wa masuala ya hifadhi ya jamii nchini
Mauritius mara baada ya waziri huyo kufungua rasmi warsha juu ya
uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii iliyoandaliwa na
taasisi ya hifadhi ya jamii ya Africa mashariki na kati (ECASSA)
inayoendelea huko nchini Mauritius.
Wajumbe wa warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya
hifadhi ya jamii kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda, Zambia,
Uganda na wenyeji Mauritius wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Fazila Jeewa waziri
wa masuala ya hifadhi ya jamii nchini Mauritius mara baada ya ufunguzi wa
warsha hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya hifadhi ya jamii ya Africa mashariki na
kati (ECASSA) juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii
inayoendelea huko nchini Mauritius.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF (kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
Washiriki
wa warsha ya Uendeshaji wa Bodi ya Mifuko ya Hifadhi Jamii
wakibadilisha mawazo. Wa pili kushoto ni, Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa
LAPF, Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Hifadhi ya Jamii ya Africa Mashariki na Kati (ECASSA) Dk. Frederic Ntimarubusa akizungumza kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Masuala ya Hifadhi ya Jamii nchini
Mauritius, Fazila Jeewa kufungua warsha inayoendelea nchini Mauritius.

