Na Chalila Kibuda
Kampuni ya Kaymu imefungua tawi lake Kariakoo
kwa ajili ya wafanyabiashara na wanunuzi kwa njia ya mtandao pamoja na uhifadhi
wa bidhaa kabla hazijasafirishwa kwenda maeneo husika, hali ambayo itasaidia
kuwapunguzia usumbufu wauzaji waliokubaliana na kampuni hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo,Meneja wa Kaymu Tanzania, Erfaan Mojgani amesema kufungua huduma kwa
njia ya mtandao ni kurahisisha uendeshaji biashara pamoja na kuondoa usumbufu
kwa mteja wa bidhaa husika.
Amesema kampuni ya Kaymu inaendesha huduma kwa
njia mtandao katika nchi 17 za Afrika ambapo wafanyabiashara wanajisajili
katika kampuni hiyo kwa ajili ya kufanya biashara kwa njia ya mtandao kwa
wateja kuchagua na kufanya manunuzi kwa bei ambayo kila mtanzania anaweza
kumudu.
Kwa upande wa Mfanyabiashara wa Viatu katika
Maduka ya kariakoo,Zacharia Lucas (Cha Classic) amesema amekuwa na mafanikio
katika kupata bidhaa kupitia Kaymu.
“Tumefurahishwa sana na hatua ya Kaymu kufungua
kituo chake hapa Kariakoo,kwani italeta mafanikio kwa wafanyabiashara kutokana
na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano”alisema Lucas.
Meneja wa Kampuni Kaymu nchini,Erfaan Mojgani
akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam,
juu ya upatikanaji wa bidhaa mbalimbali kwa njia ya Mtandao kwa wanunuzi na
wafanyabiashara katika masoko yaliyopo katika mtandao wa kaymu.
Mfanyabiashara wa Viatu katika Maduka ya
Kariakoo,Zacharia Lucas (Cha Classic) akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Dar es Salaam (hawapo pichani) juu ya faida ya kuuza bidhaa zake
katika mtandao wa Kaymu.Katikati ni Meneja wa Kampuni Kaymu nchini,Erfaan
Mojgani pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Usambazaji wa Kampuni Kaymu,Ulumbi
Bryceson.



