Waziri
wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge)Mhe.Jenista Mhagama
akisoma Muswada wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania kwa mara
ya pili katika Bunge,Mjini Dodoma.
Mhe.Lediana
Mng’ong’o Viti Maalum CCM akitoa maoni yake katika kipindi cha uchangia
wa mada kuhusu Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania,ndani ya
Bunge Mjini Dodoma.
Mbunge
wa Jimbo la Monduli, Mhe. Edward Lowassa (kushoto) akizungumza na
Mbunge wa Jimbo la Uzini, Mhe. Muhammed Seif Khatib ndani ya ukumbi wa
bunge mjini Dodoma wakati wa kikao cha Bunge.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Asha Migiro (kushoto) akimsikiliza kwa makini
Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Mwigulu Nchemba ndani ya Ukumbi wa Bunge
wakati wa kikao cha nane cha bunge.
Waziri
wa Maji Mhe.Prof.Jumanne Maghembe (wakwanza kushoto) akisalimiana na
Naibu Waziri Waziri wa Fedha Mhe.Adam Malima nje ya Ukumbi wa Bunge
mjini Dodoma,katikati ni Mhe.Lucy Nkya Mbunge wa Morogoro Vijijini.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anne Makinda
akizungumza nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma na Waziri wa Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) Mhe.Jenista Mhagama.

