baada ya mama anayeuza kilevi hicho maarufu mama Manka kulazimika kuwajia juu wateja wake wawili ambao ni makondakta wa mabasi yaendayo mikoani katika stendi kuu ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Shuhuda wa tukio hilo lililojaza watu alisema lilitokea asubuhi ya Machi 20, mwaka huu chini ya daraja jipya lililojengwa na Kampuni ya Strabag lililopo katika mradi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi ambapo makonda hao walikuwa miongoni mwa wateja waliokuwa wakinywa kinywaji hicho kinachouzwa kiasi cha shilingi elfu moja kwa kikombe.
Ghafla, zogo liliibuka baada ya mama Manka kubaini kuwa vijana wawili wanaofanya kazi kwenye mabasi yaendayo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, walikuwa wanataka kuondoka bila kumlipa fedha zake, jambo lililomfanya kuja juu, kabla ya kutulizwa na wateja wengine wakimtaka apunguze munkari ili kuzuia ‘inzi’ waliokuwa wanaanza kujaa.
Kufuatia jazba alizokuwanazo mama huyo, aliziba barabara kwa muda jambo lililosababisha kutibua usafiri Ubungo Stand.Ingawa baada ya kushtukiwa makonda hao walidai kuwa walishalipa fedha hizo, lakini baada ya mama huyo kuwaganda na kudai kutolipwa, hatimaye walilipa na kuondoka kimya kimya.

