Hapa ni katika viwanja wa Mahakama ya Mwanzo Nguzo Nane
mjini Shinyanga ambapo jioni hii kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto
Kabwe amefanya mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Sinyanga
lengo likiwa ni kunadi sera za chama hicho-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
|
Viongozi
wa ACT Wazalendo wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mkutano wa hadhara leo
jioni. |
|
Viongozi wakiwa jukwaa kuu |
|
Viongozi wa ACT Wazalendo wakiwa wamesimama |
|
Mwenyekiti wa ACT wazalendo, Anna Mughwira akizungumza na wakazi wa
Shinyanga huku wananchi wakipiga kelele kumtaka ashuke jukwaani ili ampe nafasi
Zitto Kabwe azungumze na wakazi wa Shinyanga. |
|
Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kwenye mkutano |
|
Seleman Msindi au Afande Sele akizungumza na wakazi wa Shinyanga
ambapo alisema uongozi ni akili huku akiwataka Watanzia kutoshabikia vyama vya
siasa kama mpira wa miguu kwani ni vitu viwili tofauti kwa sababu Tanzania sasa
inahitaji mabadiliko kutokana na viongozi wengi kufanya mambo kwa maslahi yao
binafsi badala ya kujali wananchi wao. |
|
Zitto Kabwe akimwaga sera za chama chake katika viwanja vya
Mahakama ya Mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine
amewaomba Watanzania kukiunga mkono chama hicho ,kukipokea na kukifanyia kazi
japokuwa mwanzo ni mgumu lakini anaamini watashinda akitolea mfano wa uchaguzi
wa serikali za mitaa chama hicho kilipata viti vingi.
|
|
Zitto
Kabwe amekanusha taarifa kuwa amemchongea mheshimiwa Reginald Mengi kwa rais
Kikwete kwamba ndiyo anachangia kuangusha serikali yake.
“Mengi
hakuhusika na sakata la Richmond,Oparesheni Tokomeza na hahusiki hata kidogo na Escrow,hizi ni chuki
tu za kutaka kunichonganisha mimi na Mengi,lakini pia kumchonganisha Rais
Kikwete na Mengi,haya magazeti ya Mawio na Taifa Imara kila siku yanatoa habari
za Zitto na ACT Wazalendo,Haiwezekani gazeti liandike habari moja wiki 6
mfululizo,Hivi hawana habari zingine za kuandika?”,-alihoji Zitto
|
|
Afande Sele akiwa na Zitto Kabwe Jukwaani. |
|
“Nimwondoe
hofu ndugu yangu Mengi hizi habari zilizoandikwa kwenye gazeti la Taifa Imara linalomilikiwa
na James Rugemarila zimetungwa,hazina kichwa wala miguu, na waliotunga ni watu
ambao wameumizwa na Escrow wanatapa tapa ,wameona waanze kuchonganisha,mchawi
wao ni wizi wao wenyewe”-alifafanua Zitto.
|
Afande Sele akifanya vituko jukwaani |
|
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano leo |
|
Afande Sele akitoa burudani kwa
wakazi wa Shinyanga |
|
Afande Sele akiwa amebebwa juu |
|
Afande Sele akiwa amebebwa na mashabiki wa muziki na wapenzi wa chama cha ACT Wazalendo |
|
Wakazi wa Shinyanga wakimshangilia Afande Sele baada ya mkutano kuisha |
|
Katikati ni Mwanaharakati Salamba Daudi Salamba
akiwasalimia wakazi wa Shinyanga baada ya kujiunga na chama cha ACT Tanzania
leo,kushoto kwake ni Mwenyekiti wa ACT Tanzania Jimbo la Shinyanga mjini-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog |