Makamu
wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akiweka shada ya maua katika
kaburi la mzee Gerald Mkude ambaye ni baba mzazi wa kiungo wa Simba,
Jonas Mkude, leo jijini Dar.
Kiungo
wa Simba, Abdi Banda (wa pili kushoto) akiwa na waombolezaji wengine
katika msiba wa mzee Gerald Mkude ambaye ni baba mzazi wa kiungo
mwenzake wa Simba, Jonas Mkude.
Kiungo
wa Simba Jonas Mkude akiwa na majonzi wakati akisikiliza misa ya ibada
katika msiba wa baba yake mzee Gerald Mkude, Konondoni jijini Dar.
Makamu wa Rais wa Simba, Kaburu akimfariji Jonas Mkude katika msiba wa baba yake, nyumbani kwao, Kinondoni Studio jijini Dar.
Viongozi
wa Simba, kutoka kushoto: Frisch Colins, Kaburu na Ally Suru wakiwa
katika Makaburi ya Kinondoni kufuatilia mazishi ya baba mzazi wa kiungo
wa timu hiyo, Jonas Mkude.
MZEE
Gerald Jonas Mkude ambaye ni baba mzazi wa kiungo mkabaji wa Simba,
Jonas Mkude amezikwa leo Jumanne jioni katika Makaburi ya Kinondoni
jijini Dar, baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo tangu Novemba mwaka
jana.
Mzee huyo
ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 46, alilazwa katika Hospitali
ya Mwananyamala tangu Alhamisi ya wiki iliyopita kabla ya Jumapili
kufariki akiwa katika hospitali hiyo ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni.
Bwana ametoa na bwana ametwaa na jina lihimidiwe, amina.
(PICHA: NASSOR GALLU/ GPL)