Floyd
Mayweather (kushoto) na Manny Pacquiao wakipozi na mkanda wa WBC jana
wakati wa mkutano na wanahabari.SIKU mbili tu zimebaki kuelekea mpambano
wa kihistoria wa ngumi za kulipwa utakaowakutanisha mabondia Floyd
Mayweather (Money) na Manny Pacquiao (Pacman) ndani ya Ukumbi wa MGM
Grand jijini Las Vegas, Marekani.
Muonekano
wa sasa wa Hoteli ya MGM Grand iliyopo jijini Las Vegas,
Marekani.Mpambano huo umekuwa gumzo kote duniani kwa sababu wapinzani
hao wamekuwa wakitafutana kwa muda mrefu kabla ya kukubali kupanda
ulingoni na kuzichapa Mei 2 mwaka huu ambapo kwa muda wa huku itakuwa
alfajiri ya Mei 3.
Money na
Pacman watakomba kiasi cha dola za Kimarekani milioni 300 sawa na zaidi
ya shilingi bilioni 589 za Kitanzania na iwapo Mayweather atashinda
pambano hilo ataweka kibindoni dola za Kimarekani milioni 180 sawa na
zaidi ya shilingi bilioni 353 za Kitanzania ambayo ni asilimia 60 ya
kiasi cha fedha kinachoshindaniwa.
ZIFUATAZO NI BAADHI YA DONDOO ZA MPAMBANO HUO:
MIKWANJA
$300
milioni - Kiasi cha mkwanja uliotengwa kwa ajili ya pambano hilo ambapo
asilimia 60 itakwenda kwa Mayweather huku asilimia 40 ikikombwa na
Pacquiao (Pacman)
$321.43 - Kiasi alichotumia Mayweather kwa upande wa vyakula wiki kadhaa akijiandaa kwa pambano hilo.
$2 - Kiasi cha fedha alizokuwa akilipwa Pacquiao kwa kila pambano wakati wa ukuaji wake huko Ufilipino
Mwanamuziki
Diddy na Mark Wahlberg waliowekeana $250,000 kwa ajili ya mpambano
huo.$250,000 - Kiasi kilichowekwa kubashiri mpambano huo kati ya
mwanamuziki Diddy na Mark Wahlberg
$600
milioni - Jumla ya kiasi cha fedha atakachokuwa ametengeneza Mayweather
kutokana na ubondia baada ya pambano lake na Pacquiao
$150 - Gharama za kuangalia pambano hilo kupitia televisheni zitakazokuwa zimefungwa katika hoteli ya MGM
£19.95 - Gharama za kuangalia pambano hilo kupitia Kituo cha Sky Sports huko Uingereza
$99.95 - Gharama ambazo watalipa mashabiki waliopo Amerika kuangalia pambano hilo kupitia HBO au Showtime
$74 milioni - Mapato yanayotarajiwa kupatikana kutokana na tiketi zilizopangiwa kiwango kati ya $1,500 na $10,000
$5.6 milioni - Kiasi kilicholipwa na Tecate kudhamini pambano hilo.
$10,000 - Malipo atakayolipwa refa wa mpambano huo, Kenny Bayless
47 - Idadi ya mapambano ya kimataifa na ushindi ambao ameupata bondia Mayweather
55.3% - Asilimia za ushindi wa Mayweather kwa knockout (KO)
62 - Idadi ya mapambano ya kimataifa aliyopigana Pacquiao
66.6% - Asilimia za ushindi wa Pacquiao kwa knockout (KO)
39 - Wastani wa makonde aliyotupa Mayweather kwa kila raundi tangu alipoanza mapambano ya kimataifa.
66 - Wastani wa makonde aliyotupa Pacquiao kwa kila raundi tangu alipoanza mapambano ya kimataifa.
74 - Jumla ya umri wa mabondia hao (Mayweather ana umri wa miaka 38 huku Pacquiao akiwa na miaka 36)
Milioni 5.8 - Idadi ya wafuasi wa Mayweather katika mtandao wa Kijamii wa Twitter; Pacquiao ana wafuasi milioni 1.8
309 -
Idadi ya maili ambazo Pacquiao alisafiri kwa basi lake la kifahari
kutoka Los Angeles kwenda Las Vegas kwa ajili ya mpambano huo.
Manny akiwa kwenye basi lake la kifahari wakati akielekea Las Vegas akitokea Los Angeles alipokuwa ameweka kambi.MPAMBANO
36 - Idadi ya dakika ambazo kila bondia atatumia kwenye ulingo iwapo pambano litachukua muda wote uliopangwa.
5 - Idadi ya miaka tangu pambano hili la kihistoria lianze kujadiliwa kwa undani.
16,500 - Idadi ya viti vya wageni wanaoruhisiwa kuingia katika Ukumbi wa MGM Grand wakati wa pambano hilo
9,000 - Idadi ya watu walioajiriwa katika Ukumbi wa MGM Grand
100,000 - Idadi ya watu wanaotarajiwa kuwepo katika hoteli ya MGM Grand kati ya Ijumaa na Jumamosi
7,000 - Idadi ya vyumba vilivyopo katika hoteli ya MGM Grand