Gazeti la The Telegraph limechapisha
stori ya aina yake leo ambapo inaripotiwa kuwa Arsenal imemfungia mama
mzazi wa nyota anayechipukia Ainsley Maitland-Niles, mwenye miaka 17,
kutohudhuria kwenye uwanja wa mazoezi baada ya kudaiwa kumshambulia kwa
maneno makali kiongozi mmoja wa Arsenal.
Kwa mujibu wa ripoti, mama huyo
anayetambulika kwa jina la Jule Niles alimtukana mtendaji wa Arsenal,
Dick Law baada ya kutishia kumtoa mwanae nje ya uwanja wakati wa mechi
ya vijana chini ya miaka 21.
The Telegraph linasema tukio
hilo lilitokea mwezi uliopita na Polisi waliitwa eneo la tukio, lakini
mama mzazi wa mchezaji huyo hajachukuliwa hatua za kisheria.
Ikiwa ni adhabu kutokana na
tabia yake mbaya, Arsenal imemfungia Mama Jule Niles kufika uwanja wa
mazoezi wa ‘London Colney training camp’.
Ainsley Maitland-Niles
aliwashitukia mashabiki wa Arsenal msimu huu pale alipopangwa kwenye
orodha ya wachezaji wa akiba wakati Arsenal inacheza ligi ya mabingwa
barani Ulaya dhidi ya Galatasaray mwezi desemba mwaka jana.
Maitland-Niles amekuwa mchezaji
wa pili kijana kuiwakilisha Arsenal kwenye mechi za ligi ya mabingwa
akiwa na miaka 17, zimepita siku 102 tu tangu afanye hivyo.