Aliyekuwa
Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za
Afrika (OAU) kuanzia mwaka 1974 hadi 1994 baada ya Afrika Kusini kupata
uhuru, Brigedia Jenerali Hashim Mbita ameaga dunia jana jijini Dar es
salaam Tanzania akiwa na umri wa miaka 74.
Nchi za kiafrika hususani
zile zilizopata uhuru kupitia katika mapambano ya kijeshi zitamkumbuka
kwa namna alivyosaidia kuondoa utawala wa kikoloni katika eneo kubwa la
bara la afrika. Kuhusu maisha ya Brigedia Jenerali Hashim Mbita
Mwanahabari wetu Arnold Kayanda amezungumza na baadhi ya waliopata kuwa
karibu na marehemu na ametutumia taarifa ifuatayo.