Watoto wawili wamekufa huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya baada ya ukuta wa nyumba waliyokuwa wamelala kuwaangukia na kuwafunika kitandani kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha mkoani Tanga.
Wakizungumza na Mpekuzi katika eneo la tukio lililopo barabara ya 18
jijijni Tanga viongozi wa serikali na wale wa wananchi wa eneo hilo
wamesema limetokea jana majira ya saa 11 Alfajiri wakati mvua iliyoambatana
na upepo ikinyesha ndipo ukuta wa nyumba hiyo uliojengwa na mawe makubwa
ya baharini ulipodondoka na kusababisha madhara hayo.
Waliokufa katika eneo hilo wametajwa kuwa ni Bakari Shabani
mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Ngamiani kati na Hassan
Abdala mwenye umri wa mwaka mmoja ambao walifariki papo hapo huku
wengine wawili wakijeruhiwa vibaya akiwemo mama mzazi wa marehemu ambao
wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.
Kufuatia hatua hiyo diwani Mbaruk ameiomba halmashauri ya jijij la
Tanga pamoja na idara ya majengo kufanya ukaguzi wa majengo chakavu hasa
katika kipindi hiki cha mvua za masika ili baadhi ya familia ziweze
kuhamishwa na kutafutiwa mahali pa kujisitiri ili kuepuka maafa makubwa
dhidi ya wahusika


