Picha
za kwanza za ndege binafsi inayotoa huduma za kihoteli zaidi angani
zimetolewa na kampuni ya Canada ikiwa ni ndege inayomilikiwa na hoteli
za
Four Seasons.
Ni ndege iliyopangwa kifahari ndani yake na
ina uwezo wa kubeba watu 52 kwa jinsi ilivyotengenezwa ndani yake na
ikawa ina nafasi kwa kila mtu kukunjua kiti chake na kukifanya kama
kitanda ambapo kama ingekua ni ndege ya kawaida nafasi hiyo ingefikisha
viti karibu 150.
Wameanza
kupokea oda za wote wanaotaka kusafiri na ndege hii kwenye nchi
mbalimbali duniani ambapo safari ya kwanza itakua mwaka 2016 kuanzia Los
Angeles na kuishia London ambapo gharama kwa kichwa ni USD 132000 zaidi ya milioni 250 za Tanzania ambazo zitajumuisha na malazi kwenye hoteli za Four Seasons kote itakapotua ambako ni Hawaii, Bora Bora, Sydney, Bali, northern Thailand, Mumbai and Istanbul.