Mamlaka
ya Nepal inasema kuwa zaidi ya watu 3300 sasa wanasemekana kufariki
katika tetemeko kubwa la ardhi siku ya jumamosi,lakini huku waokoaji
wakiendelea kuyafikia maeneo ya mashambani huenda idadi hiyo
ikaongezeka.
Mamia ya jamii zinazoishi karibu na milima zinadaiwa kuwachwa bila makao lakini harakati za kutaka kuwasaidia zinaendelea. Nepal Unicef
Shrika la umoja wa mataifa
linalosimamia watoto UNICEF limesema kuwa karibia watoto millioni moja
hawana mahala pa kulala,wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi pamoja na
mazingira safi. Huku athari zaidi za baada ya tetemeko hilo
zikionekana,wakaazi wengi waliotishiwa na tetemeko hilo katika mji wa
Kathmandu waliamua kulala nje kwa siku ya pili mfululizo ndani ya
makaazi ya mda yaliojengwa na mifuko ya plastiki.