Kiungo wa Arsenal, Hector Bellerin, akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza.
Winga wa Liverpool, Raheem Sterling, akisikitika baada ya kushindwa kuifungia timu yake bao.
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia moja ya mabao waliyofunga kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya Liverpool.
Alexies Sanchez wa Arsenal akiifungia timu yake bao.
Sanchez akishangilia kwa furaha baada ya kufunga.
Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud, akipambana na beki wa Liverpool, Kolo Toure
Staa
wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry, akiwapungia mashabiki wa timu hiyo
mkono kwenye mchezo kati ya timu hiyo na Liverpool uliopigwa kwenye
Uwanja wa Emirates.
Washika bunduki wa London, Arsenal leo wameifanyia mauaji, Liverpool
kwa kuicharaza mabao 4-1, katika mchezo wa Ligi Kuu England, uliopigwa
kwenye Uwanja wa Emirates, jijini London.
Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi ulishuhudiwa wenyeji Arsenal
wakienda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-0. Kinda Hector Bellerin
alianza kuipatia bao dakika ya 37, kabla ya Mesut Ozili kuongeza la pili
dakika tatu baadaye, kisha Alexis Sanchez kuongeza la tatu dakika ya
45.
Liver walionekana kubadilika kipindi cha pili, hasa baada ya kuingia
kwa Daniel Sturridge, ambaye mara kadhaa aliisumbua ngome ya Arsenal na
walipata penalti katika dakika ya 76 iliyofungwa na Jordan Hernderson.
Olivier Giroud alipigilia msumari wa mwisho katika dakika ya 91 na
kuifanya Arsenal ichekelee Sikukuu ya Pasaka.Ushindi huo umeifanya
Arsenal kupaa hadi nafasi ya pili na pointi 63, mbili mbele ya
Manchester City ambao watashuka dimbani Jumatatu.