Hali ya taharuki imewapata wakazi wa kijiji cha Park Nyigoti kata ya
ikoma wilaya ya Serengeti baada ya mahakama kutoa ruhusa ya kufukuliwa
kwa mwili wa Bi. Celina Jumapili aliyefariki dunia na kuzikwa tarehe
tatu marchi kisha
kuonekana utata katika kaburi lake ambalo leo limefukuliwa na kukuta sehemu ya viungovya mwili wake vimekatwa vikiwemo kiganja cha mguu vidole vya mkono wa kushoto na sehemu za siri zikiwa zimenyofolewa hali iliyozua mashaka makubwa kwa wakazi wa kijiji hicho.

Tulifika katika kijiji cha Park Nyigoti wilayani Serengeti na kushuhudia
zoezi la kufukua kaburi likiendelea ambapo inadaiwa kuwa marehemu
Celina alifariki dunia tarehe mbili ya machi na kuzikwa tarehe tatu
lakini tarehe ishirini na mbili ndugu walikuta sehemu ndogo ya kaburi
likiwa limefukuliwa ndipo wakataka kuhakiki kuwa mwili wa ndungu yao upo
au umechukuliwa. baada ya kupata kibali cha mahakama wamefukua na
kukuta viungo hivyo vikiwa vimekatwa na watu wasiyo julikana.
Akielezea namna tukio ilo lilivyo tokea mama wa marehemu Celina Bi
Nyahende Kwihamba amesema tukio hilo limewaweka katika mashaka makubwa
kutokana na kijiji hicho kushamiri kwa tabia ya ushirikina na kuiomba
serikali isaidie kumaliza tabia hiyo.