Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwahutubia wakazi wa Mtaa wa
Kilimahewa Juu iliyopo uliopo Kata ya Wazo Dar es Salaam jana, alipofika
kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu muda mrefu.
DC Makonda akizungumza na viongozi wa Manispaa ya Kinondoni na wakata ya Wazo kuhusu mgogoro huo.
DC
Makonda akisaini kwenye kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Mtaa
wa Kilimahewa Juu uliopo Kata ya Wazo jijini Dar es Salaam kuzungumza na
wananchi kuhusu mgogoro huo. Kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo,
Frank Kalinga na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Kuruthum Kazema.
Diwani
wa Kata hiyo, John Mome akizungumza katika mkutano huo kabla ya
kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ili azungumze na
wananchi.
Ofisa Tarafa wa Kawe, Nicodemus Shirika akizungumza katika mkutano huo.
Mkazi wa mtaa huo, Kauli Kibiriti akitoa ya moyoni kwenye mkutano kuhusu mgogoro wa ardhi.
Bibi Rosemary Mkasa akitoa historia ya maeneo hayo ya ardhi yanayogombaniwa.
Mkazi wa eneo hilo, Philipina Uledi naye akitoa ya moyoni kuhusu mgogoro huo.
Wananchi wa mtaa huo wakiwa kwenye mkutano huo
Mkutano ukiendelea.
Wananchi
wakishangilia wakati DC Makonda akizungumza nao ili kupata muafaka wa
mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/

