Ofisa
Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (wa
pili kutoka kushoto) akimkabidhi chetu cha uhitimu mmoja wa wahitimu wa
Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakati wa
mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni
mwa wiki. Ofisa huyo aliwakilisha wafanyakazi wa Vodacom kupitia Vodacom
Foundation ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kusaidia wasichana
katika elimu ambapo kampuni hiyo pia ilitoa msaada wa mashine ya kutoa
nakala na kuchapisha nyaraka kwa shule hiyo. Wengine ni Wajumbe wa Bodi
ya Shule.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru Rosalia Tarimo (wa
pili kutoka kushoto) akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya shule hiyo
yaliyofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Akifuatilia
ni Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia
Mutagahywa (wa kwanza kushoto) ambaye pia alikuwa ni Mgeni Rasmi katika
shughuli hiyo. Ofisa huyo aliwakilisha wafanyakazi wa Vodacom kupitia
Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kusaidia
wasichana katika elimu ambapo kampuni hiyo pia ilitoa msaada wa mashine
ya kutoa nakala na kuchapisha nyaraka kwa shule hiyo.
Ofisa
Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (wa
tatu kutoka kushoto – mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na
Wajumbe wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru na wageni
wengine waalikwa wakati wa mapokezi yake kama Mgeni Rasmi katika
mahafali ya Kidato cha Sita ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Moshi,
Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Ofisa huyo aliwakilisha wafanyakazi wa
Vodacom kupitia Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika
kusaidia wasichana katika elimu ambapo kampuni hiyo pia ilitoa msaada
wa mashine ya kutoa nakala na kuchapisha nyaraka kwa shule hiyo.
Ofisa
Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (wa
tatu kutoka kushoto) akitoa hotuba wakati wa mahafali ya Kidato cha Sita
ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakati wa yaliyofanyika
mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Ofisa huyo aliwakilisha
wafanyakazi wa Vodacom kupitia Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya
mchango wao katika kusaidia wasichana katika elimu ambapo kampuni hiyo
pia ilitoa msaada wa mashine ya kutoa nakala na kuchapisha nyaraka kwa
shule hiyo. Pamoja naye ni Mzazi Mwakilishi Cartitas Lengeju (wa kwanza
kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Paul Uria (wa pili kutoka
kushoto), Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Weruweru, Rosalia Tarimo
(wa nne kutoka kushoto) na wa tano kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya
shule hiyo.
Wasichana
wanaosoma katika shule ya sekondari ya Weruweru iliyopo mkoani
Kilimanjaro wametakiwa kufuata nyayo,kujifunza na kupata ushauri kutoka
kwa wanawake wenye mafanikio katika jamii ambao utawaongoza kwa maisha
yao ya baadaye baada ya kuhitimu masomo ya sekondari.
Ushauri
huo umetolewa na Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania
Georgia Mutagahywa katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa mahafali wa
kidato cha sita ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki
iliyohudhuriwa na wazazi,walimu na wageni kutoka sehemu mbalimbali
wakiwemo wanafunzi waliosoma shule hiyo miaka ya nyuma.
Katika
mwendelezo wake wa jitihada za kuwawezesha watoto wa kike kwenye
mahafali hayo, taasisi ya Vodacom Foundation imetoa msaada wa mashine ya
kudurufu (Photocopy) kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano
ya Vodacom Tanzania itakayorahishisha kudurufu kazi za wanafunzi na
walimu na kufanya mawasiliano na nukshi.
Vodacom
imeona kuwa mashine hii ni moja ya hitaji kubwa kwa wanafunzi wa shule
hiyo kwa kuwa itawapunguzia adha ya kupoteza muda mwingi kwenda kufuata
huduma hizo kwa umbali mrefu ambapo muda huo wangeutumia kwa masomo yao
na shughuli nyingine za kitaaluma na kwa mwaka huu imepatiwa heshima na
uongozi wa shule hiyo kutoa mgeni rasmi katika mahafali hayo ya kidato
cha sita.
Mkuu
wa shule ya Weruweru Bi.Rosalia Tarimo ameishukuru taasisi ya Vodacom
Foundation kwa msaada huo . “Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa taasisi
ya Vodacom Foundation kwa msaada huu wa mashine ya kisasa,huu ni
uthibitisho kuwa Vodacom Foundation ni kinara katika mapambano ya
kuwawezesha na kuwakomboa watoto wa kike na tunaomba taasisi nyingine
zishiriki katika kampeni ya kuwawezesha watoto wa kike”Alisema.
Safari
ya kuwakomboa watoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao bado
inakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini jitihada za kuwakomboa
zikifanyika kwa nguvu zote mafanikio yatapatikana hususani kuwafanya
watoto wa kike wapate elimu bora waweze kujiamini na moja ya njia ya
kufikia mafanikio ni kufuata nyayo,kujifunza na kupata ushauri kutoka
kwa wanawake waliofanikiwa kwenye jamii mbalimbali.
Akiongea
muda mfupi baada ya kukabidhi msaada huo,Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano
wa Vodacom Tanzania,Bi.Georgia Mutagahywa alisema Vodacom itaendelea
kusaidia shule hiyo kukabiliana na changamoto mbalimbali mojawapo ikiwa
kupitia wanafunzi waliosoma shuleni hapo. Shule hiyo pia inakabiliwa na
matatizo ya kutokuwa na mtandao wa internet ambapo Vodacom imeahidi
kulivalia njuga tatizo hilo kuhakikisha linamalizika.
“Tumetoa
msaada huu kwa shule ya Weruweru na tumekuwa tukitoa misaada ya aina
hii kwa taasisi mbalimbali kwa kuwa tunaamini kuwa kumkomboa mwanamke
ni kukomboa jamii nzima na tunaamini kuwa wanawake wakiwezeshwa na
kupata elimu bora wanaweze kuleta mabadiliko makubwa kwenye jamii yoyote
ile”.Alisema.
Taasisi
ya Vodacom Foundation iko chini ya Kampuni ya Vodacom na imekuwa
ikijishughulisha na kusaidia jamii kukabiliana na changamoto
mbalimbali hususani katika Nyanja za elimu,Afya,kiuchumi.Mwaka 2014
taasisi ya Vodacom Foundation na taasisi ya T-MARC ilizindua kampeni
inayojulikana kama ‘Msichana Kwanza’ kwa lengo la kuwawezesha wasichana
waweze kujiamini na kuwa katika mazingira bora ya kupata elimu.
Kampeni
hii imeanzia mkoani Mtwara na imeonekana kuleta mafanikio makubwa kwa
kuwa imeweza kuongeza mahudhurio ya watoto wa kike mashuleni tofauti na
hapo awali.Chini ya kampeni hii wasichana hupatiwa pedi za kuwaweka
salama wanapokuwa katika vipindi vya hedhi ambapo hapo awali wasichana
wengi walishindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa kwenye vipindi hivyo
kutokana na kutokuwepo na miundombinu mizuri na mazingira rafiki
mashuleni vilevile huweza kupatiwa elimu ya afya na uzazi ili kuwasaidia
kuepuka kupata mimba za utotoni.





