Alizaliwa
katika kijiji cha Kutama, kusini-magharibi mwa jiji kuu Harare,
alisomeshwa na wayesuti, na baadaye akawa mwalimu kabla kujiingiza
katika harakati za kupigania uhuru wa Zimbabwe.
Uwanaharakati wake ulimfanya afungwe gerezani kwa miaka 11, na baadaye mwaka 1980 akawa rais wa kwanza wa Zimbabwe.
Mugabe akionekana mwenye furaha mno
1) Zoezi na vyakula vya kienyeji
Mugabe
anapenda kufanya mazoezi. “Mimi hujihisi mgonjwa wakati sijafanya
mazoezi ya viuongo vya mwili,” Bw. Mugabe alisema miaka mitatu
iliyopita. Huwa anaamuka kati ya saa kumi na kumi na moja alfajiri, na
kutokana na jamaa zake wa karibu, husikiliza BBC idhaa ya dunia.
Siri
nyingine ya kuishi kwake kwa muda mrefu ni kuwa ywapenda sana-chakula
cha kienyeji kinacholiwa sana Zimbabwe. Kisha pia, havuti sigara, ila
hunywa pombe kidogo anapokula.
Mugabe akiwa na familia yake.
2) 'Kufufuka'
Ingawa
kumekuwa na uvumi mara nyingi kuwa Mugabe hana afya nzuri, afya yake na
kazi yake ya kisiasa yaendelea vyema kabisa. Kuhusu afya yake Mugabe
alipohojiwa wakati mmoja alisema,“ Nimekufa mara nyingi-hapo ndipo
humwelekea Yesu Kristo. Yesu alikufa mara moja, na akafufuka mara moja,”
alisema alipotimia miaka 88.
Ingawa
alilelewa katika familia ya kikatoliki-mamake alikuwa mcha
Mungu-alisema alipohojiwa na kituo cha habari cha Afrika Kusini, SABC,
miaka michache iliyopita, kuwa yeye si Mkristo anayetumikia dini kwa
sana.
3) Shabiki mkubwa sana wa kriketi
Kwa
muda mrefu amedhihirisha hadharani mapenzi ya mchezo wa kriketi. Ni
patroni wa jumuiya ya mchezo wa kriketi wa Zimbabwe, ambapo nyumba yake
ipo karibu na uga wa michezo wa Harare, ambapo anaweza kutazama kwa
makini wakati wa michezo wa kitaifa.
“Kriketi
yafanya watu wawe wangwana, na pia inawafanya watu kuwa wema,” Bw.
Mugabe alisema miaka kadhaa baada ya Zimbabwe kujinyakulia uhuru.
“Nataka kila mtu acheze kriketi Zimbabwe; nataka nchi ya Zimbabwe iwe
nchi ya wangwana.”
4) Hapendi kushindwa
Alipokuwa
kijana, Mugabe alikuwa mmakinifu na mzuri kabisa katika mchezo wa
tennis,” alisema aliyekuwa mwalimu katika shule ya Wakatoliki alikosomea
Mugabe. Ila, aliposhindwa katika mchezo huo, aliitupa raketi yake chini
kwa hasira.
Mugabe amekiri kuwa hakuwa mzuri katika mchezo wa kandanda alipokuwa mdogo, ila kwa sasa, anapenda kuutazama mchezo huo.
Yeye
ni shabiki wa vilabu vya Chelsea na Barcelona vilivyoko Uingereza na
Uhispania mtawalia. “ Ninapotazama kandanda, sitaki usumbufu kutoka kwa
mtu yeyote,” alisema mwaka wa 2012. “Hata mke wangu anajua mahala pa
kukaa wakati wanapofunga bao uwanjani, hata mimi pia hufunga bao kwangu
kwa kupiga mateke vitu vyovyote vilivyoko mbele yangu.”
5) Alipata mtoto akiwa miaka 73
Ana
watoto watatu na mke wake wa pili, Grace Marufu, aliyekuwa karani wake.
Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997, mwaka mmoja baada ya wao kufunga
ndoa.
Mwanawe
wa kwanza, Nhamodzenyika, alikufa kutokana na Malaria akiwa miaka
mitatu bado wakiwa Ghana. Bw. Mugabe alinyimwa ruhusa ya kuenda Accra
kuungana na mkewe kwa mazishi ya mwanawe, kwani alikuwa mfungwa wa
kisiasa wa serikali ya enzi hiyo ya Rhodesia.
6) Anampenda Cliff Richard kuliko Bob Marley
Mwanasiasa
wa Zimbabwe ambaye kwa sasa ni hayati, Edgar Tekere, alimwambia
mwandishi wa BBC, Brian Hungwe, kuwa alipokuwa akitayarisha kadhia ya
kusherehekea uhuru wa Zimbabwe 1980, Bw. Mugabe hakumtaka muimbaji Bob
Marley aalikwe kutumbuiza watu, ila alimtaka muimbaji maarufu wa
Uingereza, Cliff Richard. Pia anampenda Muimbaji, Jim Reeves.
Mugabe
anawachukia sana wanamitindo wa rasta, na waimbaji wa mitindo ya
reggae. Aliwaonya vijana wa Zimbabwe: “ Nchini Jamaica, wana uhuru wa
kutumia bhangi, na wanaume huwa wakati wote wamelewa. Hawataki kuenda
shule; wanataka tu kuimba, na kufuga rasta. Kama Zimbabwe, tusielekee
hapo.”
7) Mvaaji wa nguo maridadi
Anapenda
sana suti zinazoutosha mwili wake visawasawa na tai zinazofanana na
kitambaa. Hwavutia sana wanamitindo nchini Zimbabwe kwa mavazi yake.
Ila, mwanamitindo ambaye humshonea nguo zake ,Khalil Parbhoo anasema:
“Bado huavlia kama mabwana wa Uingereza –hivyo ndivyo anavyopenda."
8) Anamtzama Kwame Nkrumah kama kielelezo kwake
Bw. Mugabe alipata azma ya siasa akiwa Ghana alipokuwa mwalimu; mahali alipokutana na mke wake wa kwanza, Sally Hayfron.
Aliporudi
Zimbabwe, aliwaambia wananchi jinsi Ghana ilivyojinyakulia uhuru na
jinsi uhuru ni kitu kizuri. Katika mahojiano mwaka 2003, Mugabe alisema:
“Niliwaambia pia kuhusu Kwame Nkrumah jinsi alivyojitolea na kuiongoza
Ghana kupata uhuru;Kwame aliwaambia wananchi wa Ghana kuwa Ghana
haingekuwa nchi huru bila ya jitihada na kujitolea kwa kila mtu.”
9) Ni mtu mwenye shahada nyingi
Kwa
jumla, Mugabe ana shahada saba. Digrii yake ya kwanza ni kutoka katika
chuo kikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika Kusini. Alisomea digrii zake
zingine kwa njia Internet-mbili akiwa gerezani-shahada hizo ni za:
elimu, sayansi, sheria na usimamizi.
Amejitapa
kuwa na “shahada katika ujuhula” alipokuwa akivionya vyama vya kutetea
haki za wafanyakazi nchini Zimbabwe 1998 kila vilipotishia kugoma.