Mtoto mwenye umri wa miaka 13 amekamatwa usiku akiwa uchi kwa madai kuwa alikuwa akiwanga katika duka moja lililopo kijiji cha mpunguti Mkoa wa Mbeya.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa
mtoto huyo ni mzoefu kwa kuwa wafanyabiashara wamekuwa wakipotelewa na
fedha katika amzingira ya utata ambapo walitega mtego ili kubaini
upotevu huo na kumbaini akiingia kwenye duka moja ambalo linadaiwa
kuzindikwa.
Taarifa za awali kutoka kwa wakazi wa
eneo hilo zilidai kuwa mtoto huyo alikuwa anaishi na bibi
yake ambaye alimfukuza kutokana na tuhuma za ushirikiana na kukimbilia
msituni kutokana na kukosa pa kuishi.
Inasemekana mototo huyo aliishi misituni
kwa zaidi ya miezi mitano ndipo aliporejea na kuolewa lakini ndoa yake
haikudumu kutokana na maisha kuwa magumu na akaamua kuanza mbinu za
kichawi kwa kuibia watu.
Alianza kufungua kufuli za maduka kwa
kutumia kidole gumba huku akiwa uchi na alinaswa na kupelekwa kwenye
ofisi za kata ambapo anashikiliwa hadi sasa.


