mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Tanzanite one Hussein Gonga akiwa anamuonyesha Waziri wa nishati na majini George Simbachawene madini ambayo yanachibwa na kampuni yao. |
Na
Woinde Shizza,Arusha .
Serikali
imewataka wachimbaji na wanunuzi wa madini ya Tanzanite nchini, kuacha
tabia ya Utoroshaji wa madini hayo nje ya nchi huku,ikiagizwa kuachwa
kuuzwa madini ghafi.
Katika
kudhibiti biashara hiyo, serikali kwa kushirikiana na kituo cha
mikutano cha Arusha(AICC) inakusudia kuanzisha kituo cha kisasa cha
kimataifa cha ukataji wa madini hayo na kuuzwa nje.
Waziri wa nishati na majini George Simbachawene alitoa wito huo , wakati akifungua maonesho ya Kimataifa ya nne ya madini ya Vito jijini hapa yanayoendelea Mount Meru hoteli.
Waziri Simbachawene alisema, tabia utoroshaji wa madini hayo inaikosesha serikali mapato na pia inawapunguzia mapato wauzaji wa madini hayo na hivyo wote kupata hasara.
Akizungumza
juu
ya kituo mauzo ya madini hayo, alisema, kinatarajiwa kuwa cha kisasa,
kitakachokuwa na ofisi za kodi za mapato, kiwanja kidogo cha ndege na
ofisi za wauzaji na wanunuzi wa madini. Wakizungumzia
maonesho hayo, Wakurugenzi wa kampuni ya Tanzanite one, Faisal Juma na
Hussein Gonga walieleza yamekuwa na manufaa makubwa na kuongeza wanunuzi
wa madini.
Faisal
alisema kampuni yake, imeanzisha mafunzo ya kufundisha vijana kukata
madini hapa nchini ili kupunguza kuuzwa nje madini ghafi.
Naye
Gonga alisema kuwa kampuni hiyo, pia itaendelea kushirikiana na
serikali kuongeza ajira kwa vijana na pia kuzuia kutoroshwa nje madini
hayo.
Kamishina wa
madini,muhandisi Masanja amewata
wamiliki wa madini,wachimbaji pamoja na wauzaji kutojiingiza katika utoroshaji
wa madini kwakua unasababisha anguko la soko hilo kutokana na kupoteza bei
halali ya madini hayo. Alisema
serikali itaendelea kuboresha maonesho hayo, kila mwaka na kuhakikisha
Tanzania inakuwa kitovu cha biashara ya madini ya vito katika
Afrika.
Maonesho hayo, yanashirikisha zaidi ya mataifa manane na wanunuzi kutoka nchi za Ulaya na Marekani mwaka katika maonesho ya mwaka jana kiasi cha Tsh 3.4 bilioni kilipatikana
habari picha
kwa hisani ya woindeshizza blog